Siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
kutimuliwa nafasi hiyo kwa ulevi, wabunge na wasomi wameendelea kumbana
zaidi wakisema hatua hiyo ya Rais imechelewa.
Wapinzani wamekuwa
wakimtaka Rais amuondoe kwenye nafasi hiyo kutokana na kuhusishwa na
Kampuni ya Infosys ambayo ilitoa ushauri kwa Kampuni ya Lugumi
Enterprises iliyopewa zabuni ya kufunga vifaa vya kuchukua alama za
vidole (AFIS) katika vituo vya polisi.
Wakati wasomi wakisema
hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi huo ulikuwa sahihi na
swali ambalo Kitwanga hakulijibu vizuri kutokana na hali ya ulevi,
litapaswa kujibiwa upya baada ya wabunge kuomba mwongozo wa swali hilo.
Majaliwa alisema Rais ametengua uteuzi wa Kitwanga kuanzia juzi baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi.
“Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake...,”alisema Majaliwa.
Alisema uamuzi wa Rais Magufuli umefuata kanuni za utumishi wa umma ambazo zinakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.
Ingawa
Majaliwa hakutaja kanuni hiyo, Kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa
Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1) ya Kanuni za Utumishi wa
Umma za Mwaka 2003, kinasema, “Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka tabia
ambayo inavunja heshima ya utumishi wao kwa umma hata wanapokuwa nje ya
mahali pa kazi."
Tabia inayoweza kuvunja heshima hiyo inatajwa
kuwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, ulevi, kukopa kwa kiwango
ambacho hawawezi kurejesha na mwenendo mbaya na kujihusisha na vitendo
vyovyote viovu mbele ya jamii.
Bunge kuchukua hatua?
Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alipoulizwa adhabu ambazo mbunge
anaweza kupata iwapo ataingia bungeni akiwa amelewa, alisema wanaoweza
kujibu hilo ni Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serikali
bungeni na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jenister Mhagama.
Hata
hivyo, Mhagama ambaye ni Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Uratibu na Bunge, alisema hawezi kueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa
kwa kuwa tayari Rais ameshachukua uamuzi wa kutengua uteuzi huo.
“Ila Bunge lina taratibu na kanuni zake, nadhani Spika au katibu wa Bunge watakueleza vizuri,” alisema Mhagama.
Spika Job Ndugai hakupatikana kwenye simu, huku Naibu Spika simu yake iliita bila kupokewa.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema: “Kanuni
hazijaweka utaratibu wa mbunge anayeingia bungeni amelewa ila kuhusu
suala la Kitwanga ni la nidhamu ya utumishi wa umma, labda kama atafanya
jambo ambalo siyo la kawaida.”
Wabunge 'Wampa Makavu'
Wabunge 'Wampa Makavu'
Wabunge
wa CCM na upinzani nao walitoa maoni kuhusu hatua hiyo wakisema ilikuwa
haki kwa waziri kuachishwa kazi kwani alikuwa ametia aibu Serikali huku
wakimpongeza Rais Magufuli kuwa yuko makini.
Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya alisema alichokifanya Magufuli ni kizuri na kwa sababu waziri huyo alishindwa kujiwajibisha mwenyewe.
Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya alisema alichokifanya Magufuli ni kizuri na kwa sababu waziri huyo alishindwa kujiwajibisha mwenyewe.
Sakaya ambaye pia
ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), alisema kitendo cha Dk Magufuli
kumtimua mtu wake wa karibu, ni ishara tosha kuwa amedhamiria kuwasaidia
wanyonge na kuwatahadharisha mawaziri wengine kuwa makini na kazi zao.
“Huyu
waziri angeweza kujiwajibisha mwenyewe kutokana na makandokando yake,
lakini akachelewa na sasa amekutana na mkono wa Rais kwa kuwa hataki
uchafu, ni kweli jana (juzi) Kitwanga alikuwa amelewa wala siyo utani,”
alisema Sakaya.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa (CCM),
alimpongeza Rais Magufuli kwa kuona jambo hilo akisema, haiwezekani
kufanya kazi na watovu wa nidhamu hasa katika masuala ya ulevi.
Ndasa
alisema kulewa ni sehemu ya utovu wa nidhamu lakini inakuwa shida zaidi
pale viongozi wenye dhamana wanapolewa tena nyakati za kazi kwani
inakuwa ni mfano mbaya, hivyo waziri huyo amevuna alichopanda.
Ali
Saleh (Malindi – CUF) alisema Kitwanga alichelewa kuondolewa katika
nafasi yake kwani alikuwa ni miongoni mwa majipu.
Alisema waziri huyo alipaswa kuchunguzwa na Ikulu mapema baada ya kuanza kwa kelele za wapinzani, lakini watu wengi walishindwa kumpa Rais habari za ukweli kuhusu waziri wake.
Alisema kutumbuliwa kwa Kitwanga kusitafsiriwe kwa mambo ya ulevi pekee, maana wakuu wa mikoa na wilaya wataanza kufanya hivyo kwa uonevu kwa watu ambao watakuwa wamewanyima hata pombe vilabuni.
Alisema waziri huyo alipaswa kuchunguzwa na Ikulu mapema baada ya kuanza kwa kelele za wapinzani, lakini watu wengi walishindwa kumpa Rais habari za ukweli kuhusu waziri wake.
Alisema kutumbuliwa kwa Kitwanga kusitafsiriwe kwa mambo ya ulevi pekee, maana wakuu wa mikoa na wilaya wataanza kufanya hivyo kwa uonevu kwa watu ambao watakuwa wamewanyima hata pombe vilabuni.
Joel Mwaka (Chilonwa – CCM) alimpongeza Rais Magufuli
kuwa ni mtu anayeyaishi yale anayoahidi na hivyo kuwapa nafasi kubwa
Watanzania na hasa wa chini huku akitahadharisha viongozi kuacha
kuwadharau watu wa hali ya chini.
Suzan Kiwanga (Mlimba –
Chadema) aliyeanzisha sakata hilo, aliwalaumu wasaidizi wa Kitwanga pamoja
na dereva wake kwamba walishindwa kumshauri asiingie bungeni.
“Hakuwa
katika hali ya kawaida, alilewa sana jamani hadi akashindwa kujibu
swali, ningeshauri Rais aangalie sana kwa mawaziri wake kwani wengi
wanaonekana kulewa hata madaraka na kujibu maswali kwa nyodo,” alisema
Kiwanga.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema
alisema: “Eti wanadai ametumbuliwa sababu ya ulevi, hebu jiulize Waziri
wa Mambo ya Ndani ana wasaidizi, ana mlinzi ana katibu ana dereva, huyu
mtu aliyelewa kiasi hicho katibu alishindwa kumwambia maana kazi yao ni
kumsaidia waziri asifanye mambo ya aibu. Sasa utawala uliofitinika
hauwezi kusimama kamwe kuongoza taifa,” alisema Lema.
Waziri wa
Zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha alimpa pole Kitwaga akisema,
hata yeye alikuwa anakunywa ndovu akiwa waziri lakini hakuwahi
kutimuliwa.
“Namuonea huruma Kitwanga kwa sababu alikuwa haijui
CCM, kama ni pombe mbona hata mimi nilikuwa nakunywa ndovu, nakijua
chama hicho nilianzia chipukizi, hata umoja wa vijana, lakini niliamua
kutoka,” alisema Masha.
0 comments:
Post a Comment