Ufunguzi wa Hypermarket kubwa kuliko Mwanza unaendelea hivi sasa katika Mall ya Rock City Mwanza.
Hypermarket
 hii ambayo ni tawi jingine jipya la TSN linatazamiwa kuwahudumia wakazi
 wa Mwanza waliokuwa wakikosa uhondo wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu 
zikiwemo mbogamboga fresh kutoka hapa hapa nyumbani.
Akizungumza
 katika ufunguzi huo masaa machache yaliyopita Mkurugenzi wa TSN 
alisema,Tanzania Sisi Nyumbani  TSN itatoa zawadi kwa watu 100 wa mwanzo
 kufika katika uzinduzi huo. 
"Hii
 ni hatua nyingine kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata vitu fresh..
 kutoka nyumbani tena kwa bei nafuu.Tanzania Sisi Nyumbani tunahakikisha
 Watanzania wanafurahia mazao yao wenyewe...tena kwa bei ya gengeni 
katika Hypermarket hii.. Wateja wetu ni majirani zetu... karibuni sana 
TSN Hypermarket Mwanza." alisema.

Sehemu ya mpangilio wa bidhaa kwa ndani kama zinavyoonekana. 

Sehemu ya malipo kwa ndani kama inavyoonekana

Bidhaa aina ya mboga mboga fresh kabisa 

Bidhaa mbalimbali zikiwa ndani ya TSN,tayari kwa wateja kuanza 

Watu na wateja mbalimbali wamefika kujionea Hypermarket hiyo ya kisasa kabisa ndani ya jiji la Mwanza

0 comments:
Post a Comment