Chama
 Cha Mapinduzi (CM) kimewataka viongozi na wote waliotajwa katika sakata
 la mchanga wa madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola baada ya 
kutuhumiwa kulisababishia Taifa hasara kubwa ya matrilioni ya fedha 
kutokana na usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Hayo
 yalielezwa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey
 Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi 
ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
Aidha,
 Polepole alisema kuwa, chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua kwa 
wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia taifa hasara kupitia njia 
mbalimbali ikiwamo hii ya sasa ya kupitia mchanga wa madini. 
Polepole
 amesema kwa sasa chama kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi 
yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.
CCM imepongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho kwa jitihada kubwa anazofanya katika kuhakik
“Rais
 Magufuli anafanya kazi ya kuweka mifumo ya kusimamaia na kudhibiti 
shughuli za migodi ili zifanye kazi kwa mujibu wa sheria na kusimamia 
masilahi ya watanzania na kuhakikisha tunakomesha utoroshhwaji wa 
madini. Anatekeleza ilani ya CCM kifungu cha 35 kinachotaja kukomesha 
utoroshwaji madini katika nchi yetu,” alisema na kuongeza. 
“Niwahakikishie
 CCM sio serikali ya kinyonge hasa tunaposimamia masilahi mapana ya 
watanzania. Huyu John kapanda ndege amekuja kusikiliza shutuma za 
kampuni yake tanzu na tumeridhidhwa na uamuzi huu wa kampuni yake kukiri
 makossa.”
Aidha,
 Polepole alisema CCM haitasita kuchukua hatua kwa watakaothibitishwa na
 vyombo vya dola kwamba wameshiriki katika sakata hilo, kwani chama 
hicho kinaongozwa na kanuni ya uongozi na maadili na kwamba kitendo 
hicho ni kinyume na maadili ya katiba ya chama hicho.
“CCM
 inaongozwa na katiba, kanuni na sheria. Kanuni yetu ya uongozi na 
maadili inalenga kuweka msingi wa ujenzi wa jamii ya viongozi 
wanaosimamia haki, wanaochukia rushwa na kupiga vita ubadhirifu wa mali 
ya umma, hivyo kitendo hicho ni kinyume na katiba yetu. CCM  ni wadau wa
 kwanza kusubiri matokeo ya vyombo vyetu mbalimbali vya kiuchunguzi, 
ikionekana kuna shida tunazo taratibu na chama hakitasita kuchukua 
hatua,” alisema. 
Aliongeza kuwa “CCM
 inatoa rai, kwa baadhi yetu ambao wanataka kuugeuza mjadala huu muhimu 
kwa taifa letu kuwa siasa, kwa kutoa hukumu kwa viongozi wetu, wakuu wa 
nchi wa serikali na maamiri jeshi wetu wakuu wastaafu ambao wamefanya 
kazi kubwa ya ujenzi wa taifa hili,tuwaache hawa viongozi wapumzike, 
tusonge mbele kusimamia haki ya watanzania.”

0 comments:
Post a Comment