Haji Manara Msemaji
wa Klabu ya Simba aliyefungiwa na TFF, amefunguka mengine
mapya kwa Kusema bado hajakubaliana na ubingwa wa ligi kuu Tanzania
walioutwaa Yanga SC na kudai kuwa wao (Simba SC) ndiyo mabingwa wa ligi
hiyo msimu huu.
Manara
amebainisha hayo kupitia mitandao ya kijamii kwa kurusha vijembe kwa
wapinzani wao wa jadi na kudai kwamba kama Serengeti Boys waliweza
kushinda rufaa yao na kuweza kushiriki michuano ya vijana huko nchini
Gabon basi nao watashinda bila shika.
"Wabongo
bana kwa 'double standard' hawajambo, Serengeti Boys walikuwa Gabon kwa
kushinda rufaa ila Simba hawastahili....Mjiandae kiakili Gongowazi,
Simba ndiyo 'champion' msimu huu". Ameandika Manara
Tayari
Simba imewasilisha malalamiko yao kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA) wakipinga kupokwa pointi 3 na TFF baada ya kupewa na bodi ya ligi
kutokana na Kagera Sugar kumtumia mchezaji asiyestahili katika mechi
dhidi yao, ambapo Kagera Sugar ilipata ushindi wa mabao 2-1.
About Unknown
0 comments:
Post a Comment