Binti wa Miaka 35 Aliyejitokeza Kuwania Urais Nchini Rwanda Ahofia Usalama Wake.


Mwanadada Diane Rwigara, ametangaza azma yake ya kuwania Urais nchini Nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha .

Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.

Amesema, kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha, na kwamba huwezi kusema uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi.

Huyu ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza rasmi nia ya kutaka kugombea urais nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana Mpayimana Philippe aliyetangaza kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green.
Pia binti huyu amesema anahofu kubwa imemtanda kutokana na vitisho anavyovipata tangu atangaze nia hyo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: