Idadi ya watu waliofaliki dunia kwenye Ajari ya Basi la Super Shem Na Hiace(daladala) Jana Jijini Mwanza Yafikia 13,



Basi la Super Shem linalofanya safari za Mwanza kwenda  Mbeya lilipata ajari ya kugongana na hiace katika kijiji cha Hungumalwa Mwanza na kusababisha vifo vya watu  wanaodaiwa kufika 13 asubuhi hii.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wanaeleza kuwa Basi hilo liliigonga gari hiyo ndogo ambayo iliingia kwenye barabara kubwa bila ya kuwa na tahadhali, Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha tukio hilo.

 Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Monica Shija, Christina Costantine, Theresia Majenga wote wakiwa wakazi wa Kijiji cha Gulumwa wilayani Kwimba, Lwinzi Kope mkazi wa Kijiji cha Chaselwe, Mabula Magi wa Rukwa, Isaya Deogratius mkazi wa Mbande, Moses Kamel wa Kijiji cha Bupamwadomu, George Ndila mkazi wa Sangu, Kondakta wa hiace aliyefahamika kwa jina moja la Poni pamoja na mtu mmoja mwanaume, mama mmoja na mtoto ambao hawajafahamika wote wakiwa ni abira wa Hiace.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: