Serikali
imejipanga kununua ndege tatu na meli moja kwa ajili ya kuboresha
usafiri wa anga na majini katika maziwa makuu kwa mwaka wa Fedha
2016/2017.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Philip Mpango wakati akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi 2015 na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17.
“Serikali
itanunua meli moja mpya ya usafirishaji wa abiria na mizigo katika Ziwa
Victoria na ukarabati wa meli za MV Victoria, MV Butiama na MV Liemba
na kuimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikijumuisha ununuzi wa
ndege 3 mpya” alisema Waziri Mpango.
Alisema
miongoni mwa ndege hizo kuwa ni Bombardier CS300 yenye uwezo wa kubeba
abiria 100 – 150 na ndege mbili Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba
abiria 67- 88 kila moja.
Aidha,
Waziri Mpango alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kujenga na
kuboresha miundombinu wezeshi, kuboresha mazingira ya uwekezaji na
biashara, kuhamasisha ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma.
Kwa
mujibu wa Mpangpo Ili kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa Serikali
imeweka jitihada mahususi za kuongeza kasi ya kulipa fidia katika Maeneo
Maalum ya Uwekezaji (EPZs na SEZs); Benki ya Rasilimali kuongeza utoaji
wa mikopo katika sekta mbali mbali kutoka shilingi bilioni 538.7 mwaka
2015 hadi shilingi bilioni 726.9 kwa mwaka 2016.
Aliongeza
kuwa jitihada nyingine ni pamoja na kuitangaza Benki ya Maendeleo ya
Kilimo na huduma zake ili wananchi waweze kutumia fursa za mikopo
zinazopatikana katika benki hiyo na kuwezesha Kituo cha Uwekezaji
Tanzania kuwa na ardhi yenye hatimiliki kwa ajili ya kuikodisha kwa
wawekezaji wa nje.
Kwa
mujibu wa Waziri Mpango miradi mingi mikubwa itatekelezwa kwa ubia.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Biashara na Huduma
Kurasini, miradi ya Chuma-Liganga na makaa ya mawe – Mchuchuma na Mradi
wa barabara wa Dar es Salaam – Chalinze- Morogoro Express Way.
Waziri
Mpango alisema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ambayo
ilishaanzishwa ikiwa ni pamoja na nishati ukiwemo mradi wa Liquified
Natural Gas, kilimo cha mazao, mifugo, uvuvi, misitu, maji na
miundombinu ya reli na barabara.
0 comments:
Post a Comment