Taarifa zilizotoka June 26 kuelekea mchezo huo wa pili wa Kundi A lenye timu za MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe, Medeama ya Ghana na Yanga, uongozi wa klabu ya Yanga wametangaza kuwa mechi yao wameamua mashabiki waingie bure ili waweze kuishangilia timu yao.
Maamuzi hayo ya Yanga, wadau na mashabiki wa soka wanatafsiri kama ni maamuzi ya hasira na yanatajwa kuja kutokana na TFF imewakosea kuingia mkataba na Azam TV wa kurusha mechi hiyo live pasipo wao kushirikishwa, wakati wao wanaamini kuwa mechi hiyo ikioneshwa Dar es Salaam watakosa mapato.
0 comments:
Post a Comment