Habari Inayohusu Tanzania Kutengeza ndege Aina ya Helikopta Imeipa kick Nchi ya Tanzania Duniani Kote


Raia nchini Tanzania Jana waliamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linatengeza ndege .Gazeti la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi .

Gazeti la Zambia,Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.

Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: