SIMBA GUNDU GANI SIMBA! MICHUANO YA NILE BASIN NAYO YAYEYUKA


SHIRIKISHO la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahirisha michuano ya kuwania Kombe la nchi unakopita Mto Nile ‘Nile Basin Cup’.

Taarifa iliyotumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye imesema kwamba wamepata taarifa za kuahirisha michuano hiyo kutoka kwa waratibu wakiwamo wenyeji Sudan.

Taarifa imesema wamekubaliana kuahirisha mpaka hapo watakapotangaza tena, hivyo Simba iliyoteuliwa na TFF kushiriki michuano hiyo, imetaarifiwa kusubiri tarehe mpya ya mashindano.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: