Augustine
Mahiga ni moja ya maafisa waliotukuka wa usalama [mr x], ambaye rekodi
yake sio ya kutia shaka hata kidogo, katika serikali ya Magufuli ni moja
ya mawaziri waandamizi wanaoheshimika , ukiacha umri wake ambao
umesongo kiasi , uzoefu wake umekuwa msaada mkubwa sana kwenye
serikali,wengine wamesema ndio chaguo bora kabisa la rais katika baraza
la mawaziri.Amefanya kazi kama afisa mwandamizi kwenye awamu zote nne
,na sasa waziri.
Nimelazimika kufanya tathmini kutokana na matukio matatu ya hivi karibuni:-
1. Kutangazwa kama moja ya mawaziri
ambao hawajawasilisha fomu za tamko la mali , ambapo katika utetezi wake
alisema fomu alishajaza lakini hata rais alikuwa na taarifa kuwa
alikuwa anamuwakilisha mikutano mbalimbali ,mingine ambayo rais
alitakiwa kwenda.
2. Tukio la Picha ya kumdhalilisha
kama Waziri aliyejikojolea .....ambapo leo kwa masikitiko katika
Magazeti amekanusha kwa uchungu kuwa alijikojolea;' hata mimi sijui
lengo lao nini kuisambaza picha ile ,maana mimi niliona kama ulivyoona
wewe" , "sielewi lengo la walioitengeneza na kuisambaza picha ile"
3. Tukio la mke wake kurekodiwa na
kudaiwa ametukana , wakati kwenye clip hakuna tusi kama tusi ..pia
ameeleza limemuuma sana ," wewe umesikiliza hiyo clip,je umesikia neno
tusi?hilo ndio ninalojuwa kwa sasa sijui mengine yanayoendelea"
" ni kweli mama alikuwa katika
barabara ya namanga ambapo alipishana kauli na askari wa usalama ,mimi
nilifuatilia suala hilo kwa undani sana ,ninachoweza kusema sitaki
kuingia kwenye malumbano juu ya suala hili kwa kuwa limeshamalizika"
4. Kitendo cha rais Magufuli
kutangaza hadharani amemuonya waziri ambaye mke wake amehusika kumuonya
mkewe [ kwa kosa ambalo waziri kwa kinywa chake analalamika halioni kwa
mkewe" ..lakini pia ijulikane kuwa mke wake ni mtu mzima mwenye nafsi na
maamuzi yake ambayo huwezi kuyahukumu kwa mume moja kwa moja ...hata
ingekuwa mahakamani angepelekwa mke ..wake ..sasa iweje kumuonya mtu
mzima kama vile kosa limetendwa na mtoto wake wa chini ya miaka 18[
watetezi wa haki za wanawake watachukuliwa rais kamuona mke wa mahiga
kama mtoto]
5.Kitendo cha rais kuagiza Polisi
aliyemrekodi na kusambaza audio cilip ya mtuhumiwa na kumfanya ahukumiwe
..na umma bila kusikilizwa[sijui sheria zinasemaje juu ya kumrekodi mtu
bila ridhaa yake na kusambaza ] ..apandishwe cheo ..ni kama kumpiga
tena balozi mahiga kofi
sasa kwa kuhitimisha ..., haya ndio
malipo ambayo huyu waziri anastahili hata kwa kazi zote anazozifanya kwa
moyo ..na kujitoa pamoja na umri wake wa utu uzima , juzi tu kaongoza
kwa moyo kabisa akishirikiana na waziri muhongo juhudi za kuleta bomba
tanzania .
Huenda kuna watu ambao wanaona
ukaribu wa Mahiga kama mmoja wa washauri wa kutegemewa wa Magufuli ni
hatari katika kupenyeza ushawishi wao ...na kwa mwendo huu huenda
wakamkatisha Waziri Mahiga tamaa na akaamua kuacha kazi ....ni muhimu
kuwafanyia staha wasaidizi wa karibu .
0 comments:
Post a Comment