May 19
2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli
amekutana na mabalozi mbalimbali pamoja na katibu mtendaji wa SADC Ikulu
jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo.
Baadhi ya
mambo waliyozungumza ni pamoja na mpango wa kuanza ujenzi wa kiwanda
kikubwa cha kuzalisha mbolea kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2016 wilaya
ya Kilwa Mkoani Lindi.
Kiwanda
hicho kitatumia rasilimali ya gesi asilia na miamba ya matumbawe
‘coral reef’ iliyopo wilayani Kilwa, kitajengwa kwa ubia kati ya
Tanzania na nchi za Dernmark, Ujerumani na Pakstani na kitakuwa na uwezo
wa kuzalishatani 3800za mbolea kwa siku.
Rais Magufuli na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Egon Kochanke
Rais Magufuli na Balozi wa Uturuki hapa nchini Yasemin Aralp .
Rais Magufuli na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd .
Rais Magufuli na Katibu Mtendaji wa SADC Dk. Stergomena Tax
Balozi
wa Ujerumani hapa nchini Egon Kochanke akimkabidhi Kitabu kinachohusu
masuala mbalimbali ya Ujerumani Rais Magufuli mara baada ya kumaliza
mazungumzo
Rais
Magufuli, Katibu Mtendaji wa SADC , Stergomena Tax pamoja na Maafisa
wengine kutoka Ikulu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Kikanda na Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment