April 24 2016 ndio siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania, kwani ndio ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na mashabiki kushuhudia nusu fainali ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup), kwa upande wa Yanga walikuwa wageni wa Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mechi imeshindwa kumalizika baada ya mashabiki wa Coastal Union
kutoridhishwa na uchezeshaji wa refa hivyo mchezo umeshindwa kuendelea
kutokana na kuwa na giza na vurugu za mashabiki, dakika 90 za mchezo huo
ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, hivyo muamuzi akaongeza dakika 30
Bado
haijajulikana maamuzi yatakuwaje kutokana na mchezo kuvunjika kutokana
na uwanja kuwa giza lakini na hali ya usalama kuwa tete mashabiki wa
Coastal walikuwa wanafanya fujo
0 comments:
Post a Comment