Kama
ambavyo inatambulika kuwa suala la uhaba wa walimu limekuwa ni tatizo
ambalo utatuzi wake hauendani na kasi ya ongezeko la wanafunzi nchini.
Hivyo basi, kila mwaka serikali anawaajiri walimu wapya ili kutatua
changamoto hii. Hali hii imepelekea suala la ajira hasa za walimu
kujadiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii na kuulizwa sana na wahusika
kwenye mashine za usakaji hasa Google.
Hivyo basi, kumekuwa na matokeo tofautitofauti ya mijadala na ya mashine
za utafutaji/usakaji. Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Januari mwaka 2016,
Mheshimiwa Ndugu Waziri Mkuu Bwana Kasssim Majaliwa alifanya ziara ya
kikazi mkoani Ruvuma. Katika ziara hiyo, Majaliwa alikagua miradi
mbalimbali ikiwemo ya kielimu. Baada ya ziara hiyo alifanya mkutano wa
hadhara na wakazi hasa wazazi wa mkoani hapo.
Alizungumzia kuridhishwa kwake na maendeleo ya kiuchumi mkoani hapo
licha ya kuwepo na changamoto za hapa na pale. Baadae wananchi waliuliza
juu ya hatua zinazochukuliwa mpaka sasa juu ya utatuzi wa suala la
uhaba wa walimu mkoani hapo ambalo ni kubwa ukilinganishwa na mikoa
mingine hasa ya Dar es Salaam na Mwanza. Katika kulizungumzia hilo,
Majaliwa alisema, "Serilkali imejipanga kikamilifu kuhakikisha inatatua
tatizo la uhaba wa walimu hasa wale wa sayansi. Na hii inatarajiwa
kuanza kutatuliwa mapema Julai mwaka huu(2016) ambapo tutawaajiri walimu
nchi nzima tukiweka kipaumbele kwa walimu wa masomo ya sayansi na hasa
maeneo ya vijijini ambapo uhaba ni mkubwa mno."
Hivyo basi, taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikizagaa ni batili na
hazina uhakika wowote. Wahitimu wa kada hiyo wanaombwa kuwa wavumilivu
mpaka hapo taarifa rasmi zitakapotangazwa kwenye mtandao wa wizara na si
vinginevyo.
Kama unahitaji kupata mpya mpya juu ya ajira hizo, like page ya SebialyTZ au jiunge nami Sebialy sylivester wenye akaunti yangu ya facebook. Asante kwa kuisoma hii!
0 comments:
Post a Comment