Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wake
umepokea Tani 500 za Sukari, zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera
Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji
na Msambazaji P.H Shah.
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na
bei elekezi , na kusema kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa
nipamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.
Mongella
amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari
wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la
sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie
maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.
Mahitaji
ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya
kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 ukweli kwamba
itasaidia kupunguza uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa.
Hata
hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema,
tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na
kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.
Share:
0 comments:
Post a Comment